Loading...

MBUNGE WA UBUNGO "KUBENEA" KIZIMBANI TENA KWA KUPOTOSHA



MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka ya kuandika makala ya kupotosha na kusababisha hofu kwa jamii.

Kubenea, ambaye ni mbunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Dereck Mukabatunzi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Wakili Mukabatunzi alidai kuwa Julai 25, mwaka huu katika Mtaa wa Kasaba, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Kubenea alichapisha habari ya uongo inayoweza kusababisha hofu na taharuki kwa jamii au kuondoa amani.

Inadaiwa Kubenea alichapisha makala hiyo kwenye gazeti la Mwanahalisi la Julai 25 hadi 31, mwaka huu, lenye namba 349 ISSN: 1832-5432 ikiwa na kichwa cha habari “Yuko wapi atakayeiokoa Zanzibar”.

Baada ya kusomewa mashitaka, Kubenea alikana kutenda kosa hilo na upande wa Jamhuri ulidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali.


Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mwanga Mpya | Designed By BAKI NASI
Back To Top