Loading...

TANZANIA YAPATA PIGO KIONGOZI MZITO SERIKALINI AFARIKI DUNIA



 Dk. Didas Masaburi, aliyekuwa Meya wa jiji la Dar es Salaam
DK. Didas Masaburi, aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, amefariki dunia jana saa 3:30 usiku kwa shinikizo la damu, anaandika Faki Sosi.
Dk. Masaburi alifariki akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya kulazwa kwa siku tano kwenye chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na ndugu zake wa karibu na kwamba, tayari mipango mbalimbali ya kusimamia mazishi yake inaendelea kupangwa.
Dk. Masaburi aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) na pia mgombea Ubunge katika Jimbo la Ubungo kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kupitia Chama Cha Mapinduzi na kupata kura 59,514 dhidi ya Saed Kubenea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyepata kura 87,666.
Hata hivyo, baada ya matokeo hayo, Dk. Masaburi hakukubaliana nayo na kuamua kupeleka malalamiko yake mahakamani kupinga kushindwa na Kubenea, baadaye alifuta kesi hiyo.
Miongoni mwa kazi alizofanya Dk. Masaburi ndani ya CCM ni pamoja na kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVICCM) kwa Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1995.
Mwaka 2010 Dk. Masaburi alichaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kivukoni ambapo tarehe 23 Desemba mwaka huo, alichaguliwa kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.
Kabla ya mauti yake Dk. Masaburi alipelekwa India mara mbili kwa ajili ya matibabu lakini pia alikuwa akiishi na figo moja tangu mwaka 2000.


Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mwanga Mpya | Designed By BAKI NASI
Back To Top