MGOGORO ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) umeingia hatua ya pili baada ya Bodi ya Wadhamini kufungua kesi wakimtuhumu Prof. Ibrahim Lipumba, Jaji Francis Mutungi na watu 12 kwambwa, wanahujumu chama hicho, anaandika Faki Sosi.
Bodi hiyo leo imewasilisha maombi ya kufungua kesi katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam ya kuomba kibali cha kumzuia Jaji Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasas nchini kutofanya shughuli zake kinyume cha sheria.
Katika kesi hiyo, watuhumiwa ni pamoja na Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho aliyerejeshwa kwa barua ya Jaji Mutungi na watu 12 waliokuwa wanachama wa chama hicho.
Akizungumza na vyombo vya habari Juma Nassoro, wakili wa chama hicho amesema kuwa, wamewasilisha maombi hayo yaliyopelekwa kwa Eva Nkya, Msajili wa Mahakama hiyo ambapo ni ombi namba 75.
Wakili Nassoro ameeleza kuwa, katika maombi ya awali waliyowasilisha kabla ya kesi ya msingi kuanza kusikilizwa ni pamoja na mahakama kumuamuru Jaji Mutungi kutengua kauli yake ya uteuzi wa Prof. Lipumba.
Amedai kuwa, mahakama hiyo iliwahi kubainisha kazi za msajili wa vyama ambapo sio kuingilia uamuzi wa ndani ya vyama vya siasa.
Wakili Nassoro amedai kuwa, Jaji Mtungi hana mamlaka ya kutengua uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho .
Prof. Lipumba aliandika barua ya kujiuzulu uenyekiti wa chama hicho Agosti mwaka jana kwa madai ya kutoridhishwa na ujio wa Edward Lowassa ambaye baadaye aliteuliwa kuwa mgombea urais wa Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Hata hivyo, mwaka huu aliaeleza kuandika barua ya kutengua barua yake ya wali ya kuziuzulu kwa madai ya kutaka kujenga chama jambo ambalo limesababisha chama hicho kupasuka.
Wiki iliyopita, Baraza Kuu la Uongozi la CUF, katika kikao cha dharura kilichofanyika Makao Makuu ya CUF, mjini Zanzibar lilimfukuza uanachama wa chama hicho Prof. Lipumba.
“Baraza Kuu linaweka bayana kwa wanachama wa CUF, Watanzania na mamlaka zote nchini kwamba kuanzia leo, Prof. Ibrahim Lipumba hana haki ya kujihusisha kwa namna yoyote ile na shughuli zozote za chama,” ilieleza taarifa ya CUF.
Aidha taarifa hiyo ilidokeza kuwa, uamuzi huo umechukuliwa baada ya baraza hilo kuridhika na mashtaka dhidi ya Prof. Lipumba kuongoza na kusimamia kikundi cha wahuni kuvamia Ofisi Kuu ya Chama, Buguruni, Dar es Salaam tarehe 24 Septemba, 2016 mwaka huu.
“Baraza kuu limetumia uwezo wake, kwa mujibu wa Ibara ya 10 (1) (c) na kwa kura zote 43 za wajumbe wake waliohudhuria kumfukuza uanachama Prof. Ibrahim Lipumba,” ilieleza taarifa hiyo.
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out
Post a Comment