Loading...

SERIKALI HII KIBOKO UKUTA NDIO BASI TENA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe ametangaza kuwa Operesheni UKUTA iliyokuwa ifanyike Oktoba Mosi haitofanyika tena.

Mbowe amesema hayo leo baada ya kimya cha muda mrefu tangu kuahirishwa kwa maandamano Septemba Mosi. Aidha, Mbowe amesema kuwa hawatataja tarehe ya kufanya maandamano ili kutompa adui nafasi ya kujipanga. Amesisitiza kuwa maandamano yapo, ila tarehe hawataweka hadharani.

Operesheni hii ilikuwa ifanyike Septemba Mosi mwaka huu lakini iliahirishwa ili kuwapa nafasi viongozi wa dini kuweza kukutana na kujadiliana na Rais Dkt Magufuli juu ya mustakabali wa hali ya kisiasa nchini kufuatia kuzuiwa kwa shughuli mbalimbali za kisiasa.

Hadi leo viongozi wa dini bado hawajakutana na Rais Magufuli licha ya wao kueleza kuwa Rais Magufuli hajakataa kukutana nao kama inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari

HABARI NZITO: TAARIFA RASMI KUHUSU AFYA YA SPIKA MSTAAFU, SAMWEL SITTA

HALI ya afya ya Spika mstaafu, Samuel Sitta si nzuri,baada ya Serikali kumpeleka nchini Ujerumani kwa matibabu zaidi.

Habari za uhakika  zinasema Sitta alipelekwa Ujerumani juzi kwa matibabu baada ya afya yake kubadilika ghafla.

“Nilimtembelea siku moja kabla ya kupelekwa nje ya nchi, kwa kweli hali ya afya yake ilikuwa imedhoofu, namwombea Mungu amsaidia apone haraka ili arudi kuendelea na majukumu yake.

“Nimesikitishwa mno na taarifa za kuzushiwa kifo mzee wangu huyu, Mungu ni mwema najua bado anampigania uhai wake…hii tabia ya mitandao ya kijamii kumzushia mtu kifo sijui inafaidika nini.

“Mpaka anaondoka nchini kwenda matibabu natambua amekuwa asikumbuliwa mno na tatizo la miguu, sasa mimi si daktari wake siwezi kuongeza zaidi,”kilisema chanzo chetu.

Septemba 19, mwaka huu, Rais Dk. John Magufuli alimtembelea Sitta hospitalini alikolazwa kwa muda sasa kumjulia hali, kisha kumwombea dua Mungu amsaidie.

Siku iliyofuata Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa naye alimtembelea hospitalini kumjulia hali.

Sitta ameshika  nyadhifa mbalimbali, zikiwamo za Spika wa Bunge kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, uwaziri na ubunge kwa kipindi kirefu.

TUNDU LISSU KIBOKO YAO AIBUKA KIDEDEA MAHAKAMANI KISUTU AIBWAGA JAMHURI

TUNDU Lissu, Mwanasheria Mkuu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameiangusha Jamhuri katika kesi ya kumkashifu JPM iliyokuwa ikimuhusu Dennis Wilson

Wilson, mwanachama wa Chadema alishtakiwa na Jamhuri ya Tanzania katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa kuandika maneno ya kuudhi na kutaja jina la JPM katika mtandao wa kijamii.

Katika taarifa zilizotufikia muda huu kutoka Kisutu zinaeleza kuwa, mahakama hiyo imetupilia mbali kesi hiyo kutokana na washitaki (Jamhuri) kushindwa kufafanua uhalisi wa kifupisho JPM.

“Sababu ni hati magumashi ya mashtaka ambayo haikuwa na maelezo ya kutosheleza kwasababu watesi wetu (Jamhuri) hawakufafanua maana ya kifupisho ‘JPM’ ambaye ndiye walidai ameudhika na maneno ya Wilson.

“Mahakama imekubaliana na hoja yetu kwamba, JPM inaweza kuwa kifupisho cha Juma Pumba Maharage au majina yoyote yanayoanzia na JPM.

“Mahakama imewaelekeza washtaki kama wanataka kuendeleza vita yao basi walete hati ya mashtaka inayoeleweka,” amesema Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki.

Hata hivyo, baada ya mahakama kutupilia mbali shauri la Jamhuri, mshtakiwa (Wilson) alikamatwa tena.

“Tunawasubiria warudi tena mahakamani. Wakirudi tutaomba huyo JPM aliyeudhika na maneno ya Wilson aje atoe ushahidi wa kipi kilichomuudhi,” amesema Lissu

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM DEGREE 2016/2017

The following applicants have been selected to join various undergraduate degree programmes for the 2016/2017 academic year. 

The selected applicants should report at the Mwl. J.K. Nyerere Mlimani Campus on Saturday 8th October 2016 for the orientation week which will start on Monday 10th October 2016. 

Applicants selected for admission into Dar es Salaam University College of Education (DUCE) and Mkwawa University College of Education (MUCE) should report directly to the college's campuses in Chang'ombe and Iringa respectively on the same dates. 

Joining instructions and admission letters should be collected at the University campuses where one is admitted. Joining instructions and other important information can also be downloaded from the University website.

HAYA NDIYO MAPENZI FAIZA ALLY AFANYA MAAJABU KWA MBUNGE SUGU

Msanii wa filamu, Faiza Ally wakati inaelekea siku ya birthday ya mtoto wake Sasha, amefunguka na kueleza yamoyoni juu ya baba watoto wake, Mh Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.
Sugu na Faiza


Mwigizaji huyo ambaye anajipanga kuachia filamu yake mpya ‘Baby Mama Drama’ amesema ataendelea kumpenda Mh Sugu kwa kuwa bila yeye asingekuwa mama kwa sasa.

“Nakumbuka 2012 wakati kama huu nilianza kuumwa uchungu wako mwanangu. Yaani nilikua na raha toka siku baba yako aliyoniomba tuzae nilianza kukupenda kabla sijapata mimba. Nilipo pata ndio uwii nilikua natamani siku ifike tuonane mwanangu sasa ndio nika zidi kumpenda baba yako vibaya sana Hahhahahah,” aliandika Faiza Instagram.

“Nakumbuka siku moja na tumbo kubwaa baba yako akaniangalia nilikua na chupi tu hahaha nilikua niko bize nampangia nguo zake kabatini akaniambia sister du nime kukomesha nikamwambia aawapiiii huja nikomesha nafurahi Kila step ya mimba yangu. Sasha Mpenzi wangu stori ni nyingi sana siwezi kumaliza. Kiufupi tu toka Kwenye mimba yako nilikua na furaha sana mpaka siku nilio kupata.Mpaka leo na mahaba ndio yanazidi juu yako mwanangu. Baba yako ndio Kabisa nampenda mpaka sijielewi Kila niki kuangalia najua bila yeye leo hii nisinge kuwa Na furaha hahahahaaa tulishirikiana kitendo tukakupata naachaje kumpenda hehehehee. Asante baba Sasha Kwa kunifanya niwe mama. Mungu akubariki katika Kila unalo fanya uendelee kuwa hai mwanangu aendelee kuwa na baba yake, Asante dogo#asante sugu#Asante Joseph #asante mei Asante baba Sasha … Hatujaonana zaidi ya mwaka#hatuja ongea zaidi ya mwaka lkn haijawahi kupita siku sija kuzungumzia na sijawahi kukuacha kukupenda baby daddy… Nakupenda Leo#kesho Na siku zote 😉. Sasha birthdays loading,”alifafanua zaidi.

YALIYOJILI KWA PROFESA LIPUMBA

 Prof. Ibrahimu Lipumba (aliyesimama kwenye gari) akipokelawa kwa maandamano na wafuasi wake alipokuwa anarejea ofisi kwake Buguruni
JITIHADA za kuua upinzani nchini sasa zinaonekana baada ya Prof. Ibrahim Lipumba kukubali kazi ya kubomoa Chama cha Wananchi (CUF), anaandika Shaaban Matutu.
“Sikiliza, Lipumba hataki uenyekiti CUF,” ameeleza mbunge mmoja wa chama hicho na kuongeza “Lipumba anajua kama hastahili maana aliishatosa chama karibu sana na ushindi.”
Anasema, anachotaka Lipumba …….
Soma habari hii yote kwenye gazeti la MwanaHALISI la leo.
SOURCE: MWANAHALISI

MBUNGE SUGU WA MBEYA MJINI APATA PIGO



Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi. 
Mbeya. Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu (Chadema), amepata pigo baada ya mwenyekiti wa kampeni zake, Christopher Mwamsiku kufariki dunia akipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Ikonda wilayani Makete, mkoani Njombe.
Sugu akizungumza kwa simu amesema kifo cha Mwamsiku ambaye pia alikuwa katibu wake ni pigo kwake na Chadema.
Amesema alikuwa akisumbuliwa na kifua kwa takriban miezi mitatu iliyopita.

MBIVU, MBICHI MABOSI WA NSSF TAKUKURU


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imesema iko katika hatua za mwisho kukamilisha uchunguzi dhidi ya waliokuwa wakurugenzi wa idara sita za Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
 Akizungumza na Nipashe katikati ya wiki iliyopita mjini Kibaha, Mkurugenzi wa Takukuru, Valentino Mlowola, alisema taasisi inakaribia kukamilisha upelelezi wa suala hilo, baada ya wakurugenzi hao kusimamishwa na bodi ya wakurugenzi ya NSSF kwa tuhuma kadhaa, ikiwamo matumizi mabaya ya ofisi, Julai.
Mbali na wakurugenzi hao, bodi hiyo iliyokaa Julai 15 pia iliwasimamisha mameneja watano na mhandisi mmoja.
Mlowola ambaye ni Kamishna wa Polisi alikuwa akizungumza na Nipashe mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa Mahakama ya wilaya, uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassimu Mjaliwa.
"NSSF ni mali ya umma na hivyo Watanzania watajulishwa hatua zozote zitakazofikiwa," alisema Mlowola baada ya kuulizwa hatua ambayo uchunguzi wa Takukuru umefika zaidi ya siku 60 tangu upelelezi uanze.
“NSSF ni mali ya umma, tunaendelea na uchunguzi wetu na iwapo kutakuwa na jinai yoyote, hatua stahiki zitachukuliwa na umma utajulishwa kupitia vyombo vya habari.”
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara, alipoulizwa na gazeti hili kuhusu suala hilo hivi karibuni, alisema uchunguzi unaendelea kwa ushirikiano wa karibu na Takukuru.
Alisema baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo, umma utajulishwa kuhusu hatua stahiki zitakazochukuliwa dhidi ya wakurugenzi na mameneja waliosimamishwa.
Kikao cha Bodi ya Wakurugenzi ya mfuko huo kilichofanyika Juni 15, mwaka huu, chini ya uenyekiti wa Profesa Samweli Wangwe, kiliwasimamisha kazi wakurugenzi hao kwa tuhuma za kutofuata kanuni, sheria na taratibu katika uwekezaji, usimamizi wa miradi, manunuzi ya ardhi na ajira.
Waliosimamishwa ni Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi, Yacob Kidula, Mkurugenzi wa Fedha, Ludocick Mrosso na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Chiku Matessa.
Wengine ni Mkurugenzi wa Udhibiti Hasara na Majanga, Sadi Shemliwa, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Mahesabu ya Ndani, Pauline Mtunda na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Crescentius Magori.
Mameneja waliosimamishwa ni Meneja wa Utawala, Amina Abdallah, Meneja wa Uwekezaji, Abdallah Mseli na Meneja wa Miradi, Mhandisi John Msemo.
Wengine ni Mhasibu Mkuu, Davis Kalanje, Meneja Kiongozi kwa mkoa wa Temeke, Wakili Chedrick Komba na Meneja Mradi, mhandisi John Ndazi.
Uamuzi huo wa kuwasimamisha watendaji hao ulichukuliwa kutokana na taarifa za ukaguzi wa hesabu na shughuli za uendeshaji wa mfuko huo.
Kabla ya hatua hiyo ya bodi, Rais John Magufuli alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF wa zamani, Dk. Ramadhan Dau Februari 16 na kumteua kuwa balozi. Amepangiwa kwenda nchi ya Singapore mwezi huu.
Utenguzi wa Dk. Dau ulikuja siku chache baada ya taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuonyesha palikuwa na ukiukwaji wa taratibu katika miradi ya kadhaa ya NSSF.

AMA KWELI NABII HAKUBALIKA KWAO...TAZAMA RAYVAN NA HARMONIZE WALIVYOPOKELEWA BURUNDI

Aisee ama kweli nabii hakubaliki kwao,daah waliotunga huu msemo walikuwa ma generous sana kwa kweli

Licha Rayvan na Raj boy Harmonize kuonekana sio lulu kwa kiasi hicho hapa nchini lakini Burundi huwaambii kitu kuhusu hawa madogo maana walivyopokelewa utadhani ulikuwa msafara wa Barack Obama ,sasa hapo wameenda watoto je angeenda baba la baba Chibu dee Diamond Platinums ingekuaje????

MALI ZA CUF ZATOWEKA

 Professa Ibrahim Lipumba, aliyetajwa na Msajili wa vyama vya siasa kuwa Mwenyekiti halali wa CUFBAADHI ya mali za Chama cha Wananchi (CUF) hazijulikani zilipo na tayari Prof. Ibrahim Lipumba ameanza kuzisaka, anaandika Faki Sosi.
Taarifa kutoka kwa chanzo chetu ndani ya CUF zinaeleza kuwa, miongoni mwa mali hizo ni magari matano ya chama hicho.
Taarifa zaidi zinaeleza, kabla ya Prof. Lipumba kuingia Ofisi Kuu ya chama hicho zilizopo Buguruni jijini Dar es Salaam jana mchana, magari hayo yalikuwa tayari yameondolewa.
Na kwamba, juhudi za kutaka kujua magari hayo mahala yalipo zimeanza kuchukuliwa kwa Prof. Lipumba kuwasiliana na baadhi ya viongozi waliokuwa na dhamana na ofisi hiyo kabla ya jana.
“Magari kama sita hayapo ndani ya ofisi hizo, Prof. Lipumba ameanza kuuliza magari hayo yapo wapi?,” kimeeleza chanzo hicho na kuongeza;
“Alimpigia Mtatiro (Julius Mtatiro-Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la CUF) lakini alisema hajui, akampigia Paku (Abdalla Paku-Ofisa Utawala wa CUF) alikata simu na alimpigia Bashange (Joram Bashange Mkurugenzi wa Fedha wa CUF) alimjibu kuwa yupo mkoani.”
Hata hivyo, mtandao huu umemtafuta Abdul Kambaya anayetajwa kuwa mtu wa karibu na Prof. Lipumba ambaye amethibitisha taarifa hizo.
“Ni kweli magari hayapo na Profesa amekuwa akifanya juhudi za kutaka kujua magari hayo yalipo.
“Bado hatujaangalia mambo mengine zaidi lakini kuna baadhi ya vitu havipo na tutaendelea kuangalia mali ipi ya chama na nani anayo,” amesema Kambaya na kuongeza;
“Mali za CUF ni za wanachama wote na hakuna shaka tutajua zilipo. Hatuamini kama zimetoka nje kwa njia za hovyo ila naamini mwenyekiti anataka kujua tu mali hizo zipo wapi kwa kuwa anawajibuka kujua.”
Kambaya amebainishwa kwamba, Prof. Lipumba amekuwa akiwasiliana na baadhi ya viongozi ili kutaka kujua yalipo magari hayo.
“Sijui kwa watu wengine lakini najua kuwa amewasiliana na Bashange ambaye alijibu kwamba yupo nje ya Dar es Salaam,” amesema Kambaya.
Jana kwenye Ofisi Kuu ya chama hicho kulikuwa na hekaheka kutokana na Prof. Lipumba kurejea ofisini hapo akisindikizwa na wafuasi wake.
Hatua hiyo iliyokana na taarifa ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini iliyotolewa jana ikieleza kumtambua Prof. Lipumba kwamba ni mwenyekiti halali wa chama hicho kwa mujibu wa taratibu.
“Baada ya upembuzi wangu ni kuwa, Lipumba bado mwenyekiti halali wa CUF na waliofukuzwa, kusimamishwa ni wanachama halali.
“Viongozi ambao uamuzi wao uliathirika na maamuzi ya Baraza Kuu la Uongozi wa Taifa bado ni viongozi halali wa CUF,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.
Prof. Lipumba aliandika barua ya kujiuzulu uenyekiti wa chama hicho Agosti mwaka jana kwa madai ya kutoridhishwa na ujio wa Edward Lowassa ambaye baadaye aliteuliwa kuwa mgombea urais wa Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Hata hivyo, Agosti mwaka huu CUF ilimsimamishwa uanachama Prof. Lipumba kwa tuhuma za kuwa kinara wa vurugu zilizosababisha mkutano mkuu maalum wa chama hicho kuvunjika.
Mkutano huo ulifanyika katika Hotel ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam, Prof. Lipumba na wafuasi wake waliuvamia na kusababisha kuvunjika.
Wengine ni Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Kaliua; Maftaha Nachuma, Mbunge wa Mtwara Mjini na Kambaya.
Uamuzi huo ulitangazwa rasmi Nassor Ahmed Mazrui, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, wakati akitoa taarifa ya Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi Taifa (BKUT), kilichofanyika mjini Zanzibar mwezi uliopita.

HABARI NZITO: LIPUMBA SASA AFUNGUKA MAMBO MAKUBWA AMAKWELI ALIKUWA NA SIRI NZITO

Prof. Ibrahim Lipumba
BAADA ya kuingia Ofisi Kuu za Chama cha Wananchi (CUF), Buguruni jijini Dar es Salaam, mchana wa jana Profesa Ibrahim Lipumba amezungumza mambo mbalimbali kuhusiana na kurejeshwa kwake na Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama Vya siasa hapa nchini, anaandika Charles William.
Prof. Lipumba alikuwa mwenyekiti wa CUF kabla ya kuandika barua ya kujiuzulu tarehe 05 Agosti mwaka jana, lakini tarehe 08 Juni mwaka huu aliandika barua ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu na kuzua mvutano ndani ya chama hicho.
Mapema baada ya kupata barua ya Jaji Mutungi inayoeleza kumtambua kama mwenyekiti halali wa CUF Lipumba aliwasili Ofisi Kuu za chama hicho na kusema yupo tayari kukitumikia tena chama hicho.
“Nimerejea tena na nitafanya kazi kwa ari, sikukutana na Maalim Seif barabarani. Nimekutana naye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1973. Tena tulikutana  msikitini,” amesema.
Akizungumza kuhusu kuomba kurejea baada ya kujiuzulu, Prof. Lipumba amesema, “wazee na viongozi wa dini waliniomba nirejee, nikawasikiliza, nikawambia nitarejea ila wazungumze kwanza na Katibu Mkuu. Wakaenda kwa Maalim, akawajibu; hana tatizo na mimi, wazee wakaniambia Maalim hana tatizo na wewe.”
Prof. Lipumba amesema, aliandika barua ya kurejea tarehe 08 Juni mwaka huu, akimtaarifu Maalim Seif kuwa, angeanza kazi ya uwenyekiti tarehe 10 Juni, na kwamba kazi yake ya kwanza ingekuwa kuchambua bajeti ya nchi.
“Tarehe 09/06 Katibu mkuuu akaniambia nisianze kwanza kazi mpaka ashauriane na wanasheria. Nikamjibu kuwa nazingatia ushauri wake lakini hakuna utata wa kisheria kwasababu Katiba inasema wazi kuwa, kujiuzulu ni mpaka ithibitishwe na mamlaka iliyokuchagua.
Baadaye nikasikia akisema kuwa maamuzi ya chama yatafanywa kwenye vikao. Kiukweli hata mimi sikupenda tufikie tulipofika. Hata hivyo kwa kuwa msajili katoa maelekezo ambayo ni lazima yafuatwe naomba sasa tusahau yaliyopita na tugange yajayo,” ameeleza.
Lipumba amesema anataka kujenga mtandao wa chama hicho ili chama kienee nchi nzima na kusisitiza kuwa atafanya kazi na viongozi wote waliochaguliwa kihalali lakini siyo wale walioteuliwa 28 Agosti mwaka huu na Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho.
“Katika mvutano huu, hakuna aliyeshinda. Iliyoshinda ni Katiba ya CUF na sisi lazima tukubaliane na ukweli huu. Ni aibu kwa chama cha haki sawa kwa wote kufanya mambo bila kuzingatia demokrasia,” amesema.
Lipumba pia ameeleza masikitiko yake kwa chama cha CUF kutoka kuwafukuza wabunge wa kuchaguliwa Magdalena Sakaya (Kaliua) na Maftah Nachuma (Mtwara).
“Haiwezekani ufukuze wabunge. Sakaya ni mwanamke pekee wa CUF aliyeshinda jimbo kwa upande wa Bara, jimbo lake la Kaliua ni kubwa kuliko hata Zanzibar lakini alipambana na kushinda, leo tunamfukuza ili tumpoteze kirahisi? Huyu ni kipenzi cha wananchi wa Kaliua.
Unamfukuza Maftah? Ukizungumzia watu ngangari kinoma ndani ya CUF huwezi kuacha kumtaja Maftah, alisimama katika uchaguzi mkuu mwaka jana na NCCR, Chadema na CCM lakini akawagaragaza, leo tunamfukuza. Tutaingiaje Kusini? Tutaingiaje Mtwara?” ameng’aka.
Lipumba amesema alisikitishwa na wanachama waliokuwa wakimshambulia kwa nyakati tofauti akiwemo Julius Mtatiro na Hamidu Bobali, Mbunge wa Jimbo la Mchinga mkoani Lindi.
“Bobali anaendesha vikao vya kumfukuza Maftah na kunibeza mimi, huyu ni kijana niliyemlea na kumpeleka Ulaya mwaka 2014 lakini amekengeuka. Mtatiro nimemteua mimi kuwa Naibu Katibu Mkuu na baadaye Mjumbe wa mkutano mkuu lakini alikuwa akinishambulia, jambo hili linasikitisha sana,” amesema.
Prof. Lipumba amewataka viongozi wote waliowekwa madarakani na Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho mwezi mmoja uliopita kukaa kando vinginevyo watajikuta wakifikishwa katika vyombo vya sheria.
“Msajili ameweka msisitizo kuwa mtu yoyote asijifanye kiongozi wakati si kionggozi vinginevyo atatozwa faini milioni moja au kufungwa miezi sita au vyote kwa pamoja.
Wakati CCM na Magufuli wakisema Hapa Kazi Tu sisi lazima tusimame katika falsafa ya Hapa Haki Tu,” Amehitimisha Prof. Lipumba.

HAPATOSHI TENA PROFESA LIPUMBA ATANGAZWA RASMI KUWA MWENYEKITI WA CUF

 Prof. Ibrahim Lipumba  akiwa na wafuasi wake
PROFESA Ibrahim Lipumba, aliyetangazwa kusimamishwa uanachama na Chama cha Wananchi (CUF), ametangazwa kuwa mwenyekiti halali wa chama hicho, anaandika Faki Sosi.
Taarifa ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini iliyotolewa jana na kusambazwa leo imeeleza kuwa, Prof. Lipumba bado ni mwenyekiti wa chama hicho kwa mujibu wa taratibu.
“Baada ya upembuzi wangu ni kuwa, Lipumba bado mwenyekiti halali wa CUF na waliofukuzwa, kusimamishwa ni wanachama halali.
“Viongozi ambao uamuzi wao uliathirika na maamuzi ya Baraza Kuu la Uongozi wa Taifa bado ni viongozi halali wa CUF,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa Jaji Francies Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.
Prof. Lipumba aliandika barua ya kujiuzulu uenyekiti wa chama hicho Agosti mwaka jana kwa madai ya kutoridhishwa na ujio wa Edward Lowassa ambaye baadaye aliteuliwa kuwa mgombea urais wa Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Katika Ofisi Kuu ya chama hicho iliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam, wafuasi wa Prof. Lipumba mchana huu wamefurika wakimsubiri na kwamba, yupo njiani kwenda ‘ofisini kwake.’
Agosti mwaka huu CUF ilimsimamishwa uanachama Prof. Lipumba kwa tuhuma za kuwa kinara wa vurugu zilizosababisha mkutano mkuu maalum wa chama hicho kuvunjika.
Mkutano huo ulifanyika katika Hotel ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam, Prof. Lipumbana wafuasi wake waliuvamia na kusababisha kuvunjika.
Pamoja naye katika adhabu hiyo ni viongozi waandamizi wengine 10 akiwemo Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Kaliua; Maftaha Nachuma, Mbunge wa Mtwara Mjini na Abdul Kambaya, Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma.
Uamuzi huo ulitangazwa rasmi Nassor Ahmed Mazrui, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, wakati akitoa taarifa ya Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi Taifa (BKUT), kilichofanyika mjini Zanzibar mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi wengine waliochukuliwa hatua hiyo hadi watakapojieleza mbele ya Baraza Kuu hilo, ni Ashura Mustafa, Omar Mhina Masoud, Thomas Malima, Kapasha M. Kapasha, Mohamed Habib Mnyaa, Haroub Shamis na Mussa Haji Kombo.
Wakati Ashura ni mjumbe wa Baraza Kuu na mwanamama aliyewahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma wa chama, Mnyaa na Kombo ni viongozi wazoefu waliokuwa wabunge kipindi cha 2010/2015; Mnyaa akiwakilisha Jimbo la Mkanyageni na Kombo Jimbo la Chake Chake, kisiwani Pemba.

KUFULI ZAVUNJWA, RISASI ZARINDIMA CHAMA CHA WANANCHI (CUF)

Picha ndogo mbili za kwanza zinaonesha hali ilivyokua wakati Professa Ibrahim Lipumba akiwasili ofisi za Chama cha Wananchi (CUF) baada ya Msajili wa vyama vya Siasa kumthibitisha kuwa ni Mwenyekiti halali wa chama hicho
RISASI za moto zimerindima katika Ofisi Kuu ya Chama cha Wananchi (CUF) Buguruni, jijini Dar es Salaam leo mchana, wakati Prof. Ibrahim Lipumba alipowasili ili kuanza rasmi kazi baada ya kupokea barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa inayomtambua kuwa mwenyekiti halali wa chama hicho, anaandika Charles William.
Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, katika barua yake iliyoandikwa 23 Septemba mwaka huu, ameeleza kumtambua Prof. Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa CUF na kwamba, viongozi wa CUF walioteuliwa na Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho 28 Agosti mwaka huu si halali.
Katika mapokezi yake, wafuasi wa Prof. Lipumba walijipanga kuanzia Barabara ya Buguruni (Rozana) inayoingia Ofisi Kuu za chama hicho na kuimba huku wakipuliza matarumbeta. Ilikuwa saa 7:00 mchana ambapo dakika ishirini na mbili baadaye kiongozi huyo alifika katika barabara hiyo akiwa katika gari aina ya Rav 4 yenye Na. T 639 AZK.
Baada ya wafuasi wake kumlaki, Prof. Lipumba alishuka na kuanza kutembea kwa mguu sambamba na wafuasi wake hadi ofisi za chama hicho zilizopo umbali wa takribani mita 300 kutoka barabarani hapo.
Wafausi hao walimsindikiza wakiimba nyimbo mbalimbali za chama hicho ikiwemo nyimbo yao maarufu, “Ooooh chamaaa… chama gani? Chama cha Wananchi CUF, Oooh chamaaa… chama gani? Chama cha Wananchi CUF.”
Walikutana na kundi lingine kubwa katika ofisi hiyo, hata hivyo geti la lango kuu lilikuwa limefungwa hivyo Prof. Lipumba alishindwa kuingia.
Baada ya kupita dakika tano tangu kuwasili Prof. Lipumba katika eneo hilo, zaidi ya wafuasi wake 20 waliparamia ukuta na kuingia ndani ya ofisi hiyo kisha kuwakabili walinzi waliokuwa wamefunga geti hilo na kisha walilivunja.
Baada ya walinzi kuzidiwa nguvu, walikimbia kwa kuruka ukuta na kudondokea nyumba za jirani na kutokomea, mmoja wa walinzi hao alinyang’anywa bunduki na wafuasi hao. Baada ya kuvunjwa kufuli la geti la lango kuu, Prof. Lipumba na kundi kubwa la wafuasi wake waliingia ndani huku wakishangilia.
Wakati hayo yakitendeka, polisi walikuwa nje ya ukuta wa ofisi hiyo ndani ya gari lao lenye namba PT 3699 wakiwa na silaha za moto. walikuwa watulivu ndani ya gari hiyo bila kuchukua hatua zozote. Baada ya muda mchache gari nyingine ya polisi yenye Na. T 709 ASF iliwasili ili kuongeza ulinzi.
Mara baada ya Prof. Lipumba kuingia ndani, polisi nao waliingia ndani kwa lengo la kuichukua bunduki iliyokuwa mikononi mwa wafuasi wa Lipumba. Wakati huo risasi za moto zilipigwa hewani kutokana na sintofahamu iliyokuwepo eneo hilo.
Hata hivyo, Prof. Lipumba hakuweza kuingia ndani ya ofisi kutokana na mlango wa kuingia ndani kufungwa, wafuasi waliamua kuvunja kufuli kwa nguvu chini ya usimamizi wa polisi na hatimaye aliingia ndani.
Mkuu wa askari hao aliokuwa amevaa kiraia sambamba na mwingine mwenye jina MADALI S.B walishuhudia tukio hilo, katika hali ya kushangaza askari aliyevalia kirai aliyeonekana kuwa kiongozi w polisi hao, alitishia kuvunja kamera za wandishi wa habari watakaompiga picha.
Prof. Lipumba aliingia ndani ya ofisi yake na kuzungumza na waandishi wa habari akisema, “nimerejea kazini na nawasihi wana CUF wawe wamoja, wasahau yaliyopita tukijenge chama chetu.”
Lipumba aliongea kwa muda mfupi na waaandishi hao kabla ya kutoka nje kuzungumza na wafuasi wake, ambapo amewatahadharisha viongozi wa muda waliowekwa na kikao cha baraza kuu la chama hicho 28 Agosti mwaka huu kukaa mbali na shughuli za chama hicho.
Lipumba amesema, “Nataka kujenga chama kitakachoenea kila mahali si chama cha upande mmoja tu, sina tatizo na viongozi wa CUF waliochaguliwa na wanachama katika uchaguzi mkuu.”
Pof. Lipumba aliwaaga wanachama wake na kuwasihi kumpa ushirikiano ili aweze kukijenga chama hicho. Hata hivyo katika hali ya kushangaza gari yake aliyokuja nayo Na. T 639 AZK iligoma kuwaka nay eye kushindwa kuondoka katika eneo hilo.
Tukio hilo lilitokea saa nane na dakika arobaini mchana (8:40) na ilimlazimu Prof. Lipumba kukaa kwa zaidi ya dakika 10 gari hilo liweze kuwashwa, lakini halikuweza kuwaka na hivyo kulazimika kupanda gari linguine Na. T 581 CJU ambalo lilikuwepo katika eneo hilo.
Haikujulikana mara moja gari hiyo ni mali ya nani, Prof. Lipumba aliondoka katika eneo hilo huku ndani ya gari hiyo akiwa ameambatana na watu wengine wanne na magari matatu yenye askari polisi yakimsindikiza nyumba.
Magari yaliyomsindikiza nyuma wakati Prof. Lipumba akiondoka katika eneo la ofisi kuu za  CUF, Buguruni  majira ya saa nane na dakika hamsini (8:50) ni pamoja na lile lenye namba za usajili PT 3891, PT 3699 na T 709 ASF.
Hata hivyo taarifa ambazo MwanaHALISI online imezipata, zinaeleza kwamba gari hizo za polisi zilienda kumzuia Prof. Lipumba katika eneo la barabara kuu na kumtaka afike Kituo cha Polisi Buguruni kwa mahojiano ambapo alitii na kuhojiwa kabla ya kuachiwa.
Hivi punde tutakuletea kwa kirefu kile alichoongea Prof. Lipumba mbele ya wafuasi wake.
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mwanga Mpya | Designed By BAKI NASI
Back To Top