Loading...

HABARI NZITO: RAIS JPM KIBOKO MHADHIRI WA CHUO KIKUU CHA MKWAWA (MUCE) AKAMATWA KWA KUMKASHFU RAIS JPM





Rais John Magufuli  
Iringa.Idadi ya watu wanaokamatwa kwa tuhuma za kumkashfu Rais John Magufuli kupitia mitandao ya kijamii imezidi kuongezeka baada ya polisi kumkamata Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Mkwawa (Muce), Dk Oscar Magava (48).
Dk Magava amekuwa mtu wa kumi kukamatwa na polisi katika kampeni za jeshi hilo kudhibiti uhalifu chini ya sheria ya uhalifu wa mtandaoni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi alisema Dk Magava alikamatwa akiwa Sumbawanga na alirudishwa mkoani Iringa.
Mjengi alisema Septemba 15, mwaka huu walipata taarifa kuwa mhadhiri huyo anatumia mitandao ya kijamii kumkashfu Rais. Alisema waliamua kumsaka na walipopata taarifa kuwa Dk Magava amekwenda Sumbawanga waliwasiliana na polisi wa huko wakamkamata na kumrudisha Iringa.
Hata hivyo, Kamanda Mjengi hakuyataja maneno aliyotumia Dk Magava kumkashfu Rais kwa madai kuwa bado wanaendelea na uchunguzi na kwamba ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Kamanda Mjengi aliwatahadharisha wananchi kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kuitumia kwa ajili ya maendeleo na si kutukana wala kukashfu viongozi au watu wengine.
Watu mbalimbali wamekuwa wakikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kumkashifu Rais au jeshi la polisi.
Ajali ya gari
Katika hatua nyingine, Kamanda Mjengi alisema watu watatu wamekufa papo hapo huku wawili wakijeruhiwa baada ya gari dogo walilokuwa wakisafiria kutumbukia kwenye mtaro katika barabara ya Iringa-Mbeya.
Kamanda Mjengi aliwataja waliokufa kwenye ajali hiyo kuwa ni Hassan Mbuyu (35), William Simon (30) wote wakazi wa Dar es Salaam na Mariana Mayemba (25) mkazi wa Makambako mkoani Njombe.Waliojeruhiwa ni Jackline Mwakyokile mkazi wa Mbeya na Francis Yangison.
Alisema ajali hiyo ilitokea eneo la Nzivi wilayani Mufindi ambako gari aina ya Toyota Allion mali ya kampuni ya Excellent lililokuwa likiendeshwa na Francis Yangison lilipotumbukia kwenye mtaro wa barabara hiyo inayojengwa.
Kamanda Mjengi alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kwa kutozingatia alama za barabarani.


Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mwanga Mpya | Designed By BAKI NASI
Back To Top