MGOGORO unaonukia kati ya Chama cha Wananchi (CUF) na Profesa Ibrahimu Lipumba kuhusiana na nafasi ya uenyekiti wa taifa umechukua sura mpya
baada ya chama hicho kumtuhumu mambo mapya kadhaa mgombea wao huyo wa zamani wa nafasi ya urais ikiwamo kula njama za kutaka kukiangamiza na pia kumhusisha na fedha za michango kiasi cha Sh. milioni 280.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Taifa wa CUF, Julius Mtatiro, ndiye aliyetoa tuhuma hizo nzito dhidi ya Lipumba wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
“Tuna ushahidi… tunaweza kuweka kila kitu hadharani. Anataka kukiua chama cha CUF kilicho na wabunge 43, madiwani 300 na wenyeviti wa mitaa 1,000,” alisema Mtatiro.
Aliongeza vilevile kuwa Lipumba aliwahi kuchangiwa Sh. milioni 280 na baadhi ya wabunge wa chama chao (CUF) ili zisaidie mchakato wake wa kugombea urais katika uchaguzi mkuu na kwamba, inashangaza kuona kuwa sasa anaongoza njama za kukiangamiza chama cha wabunge hao.
“Ni wabunge hao hao, baadhi yao ndiyo walimchangia Sh. milioni 280 ili agombee urais,” alisema Mtatiro.
Mtatiro aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara) chini ya uenyekiti wa Lipumba, alidai kuwa (Lipumba) amekuwa akifanya vikao vya kila mara nyumbani kwake ili kupanga njama za kuiua CUF.
Hata hivyo, Nipashe haikuweza kuthibitisha ukweli wa madai ya Mtatiro juu ya Lipumba kupitia vyanzo vilivyo huru.
Aidha, jitihada za kumtafuta Lipumba ili azungumzie tuhuma hizo na nyingine za CUF dhidi yake jana ziligonga mwamba baada ya kutopatikana.
Simu yake ya mkononi iliita muda wote bila kupokewa na pia hakukuwa na majibu kutokana na swali aliloulizwa kuhusiana na suala hilo kupitia ujumbe mfupi katika simu yake ya mkononi.
Lipumba aliyesimamishwa uanachama hivi karibuni pamoja na wafuasi wake kadhaa kutoka miongoni mwa wanachama wa CUF, anavutana na chama hicho kuhusiana na nafasi ya uenyekiti.
Aliingia katika mgogoro baada ya kuwahi kuandika barua ya kujiuzulu muda siku chache kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015 na kisha kuandika barua nyingine baadaye ya kutaka barua yake ya awali isitambuliwe ili aendelee kukiongoza chama hicho.
Lipumba anasisitiza kuwa bado yeye ni mwenyekiti halali wa chama hicho kutokana na barua aliyoiandika ya kusitisha tangazo lake la awali, lakini uongozi wa juu wa CUF unapinga jambo hilo kwa kudai kuwa katiba yao haimpi fursa hiyo, hasa baada ya kusudio lake kukataliwa na wajumbe zaidi ya 470 (zaidi ya asilimia 70) katika mkutano mkuu uliofanyika Agosti 22, mwaka huu kabla ya kuvunjika.
Wakati alipotangaza kujiuzulu, Lipumba alisema sababu ya kufanya hivyo ni kutounga mkono kukaribishwa kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, katika muungano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Umoja huo (Ukawa) huundwa na Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD.
BASHANGE ASIMULIA MKASA KUTEKWA
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha wa chama hicho, Joram Bashange alisimulia jaribio la kutaka kutekwa na kulihusisha na mvutano unaoendelea ndani ya cham chao .
Bashange alisema tukio hilo lilijiri majira ya asubuhi akitoka nyumbani kwake mtaa wa Madenge, Buguruni jijini Dar es Salaam, alishangaaa gari nyeusi aina ya Noah (namba tunazo) ikipaki mbele yake.
Alisema kuwa gari hiyo ilikuwa na watu wanne na mmoja wao alifungua mlango kabla ya kumvuta kwa nguvu ili aingie ndani ya gari hiyo.
“Baada ya kutembea hatua 20 kutoka nyumbani kwangu, Noah ilipaki mbele yangu na kunilazimisha kuingia ndani ya gari… watu hao wote ninawajua,” alisema Bashange, huku akiwataja majina watu hao ambao mmoja wao alifanikiwa kukimbia.
Alieleza kuwa, wakati vuta nikuvute ya kumuingiza ndani ya gari ikiendelea, watu waliokuwa jirani walilizingira gari hilo na hatimaye kutibua mpango huo huku wakiwezesha kukamatwa kwa wahusika kabla ya kufikishwa katika kituo cha Polisi Buguruni.
Alisema kuwa mmoja wa watu hao alipokaguliwa kituoni alibainika kuwa na pingu, na kwamba walifunguliwa jalada namba BUG/IR/5937/2016.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salim Rashid, aliithibitishia Nipashe kutokea kwa tukio hilo, pamoja na kuwashikilia watu watatu kwa tuhuma za kutaka kumteka Bashange.
Alisema uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea na kwamba utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out
Post a Comment